Friday, July 13, 2012
BAADA YA TREY SONGZ - JASON DERULO KUTUA RWANDA
List ya mastaa toka unyamwezini kuja kuperform ndani ya bara la Afrika inazidi kuongezeka kila kukicha.
Baada ya Trey Songs kualikwa na prezidaa wa Rwanda kwa ajili ya kutumbuiza kwenye bday party ya his son, round hii ni zamu ya star wa ngoma ya "Watcha Say" kuwapagawisha Warwanda.
Jason Derulo ambaye atawasili nchini humo tarehe 27, atakuwa mtumbuizaji mkubwa kwenye fainali za shindano kubwa la muziki nchini Rwanda, lijulikanalo kwa jina la Primus Guma Guma Superstar ambalo linafanyika kwa mara ya pili nchini humo.
Tarene 29 ya mwezi huu, ndiyo siku ambayo Derulo ata-hit stage moja na wasanii wakubwa wa Rwanda, ambapo wasanii hao wa nchini Rwanda watachuana ili kumpata staa mkubwa wa ukweli kutoka nchini humo, miongoni mwa wale wanaowika.
Mwaka jana, shindano hilo lilifanyika na mwanamuziki wa R&B nchini humo Tom Close, aliibuka mshindi.
Tofauti ya shindano hili na mashindano kama BSS na Tusker Project Fame, ni kwamba lenyewe hushindanisha wasanii waliofanikiwa tayari na wasanii kumi pekee ndio huchaguliwa kushiriki, kama ilivyokuwa kwa Mfalme wa Rhymes Tanzania.
Wasanii hao hutumia nyimbo zao wenyewe wakati wa shindano hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment