WEMA AITWA IKULU YA BURUNDI
Wema Sepetu
WEMA Isaac Sepetu amelidokeza gazeti alipendalo la Ijumaa Wikienda kuwa ameitwa ikulu ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kwa mwaliko. Wema alisema mwaliko huo aliupata mara tu baada ya kuzindua ile filamu yake ya Super Star wiki mbili zilizopita ambapo katika mwaliko huo wa ujumbe kutoka ikulu hiyo ulimuomba kutoisambaza kwanza kabla ya kwenda kuizindua nchini humo.
“Waliniambia juu ya mimi kuomba uraia wa nchi hiyo ili kukuza filamu zao. Kusema kweli nilikuwa nina ratiba ya kwenda kuizindua filamu yangu Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yaani sijui hata walijuaje. Sijui ni nini kimetokea, nina wasiwasi. Hata sijui nitaongea nini na Rais wa Burundi,” alisema Wema na kuongeza kuwa maandalizi yakikamilika atatii wito huo muda wowote
No comments:
Post a Comment