Wednesday, June 27, 2012

UMRI WA LULU SERIKALI YAENDA MAHAKAMA YA RUFAA




Upande wa mashitaka katika suala la utata wa umri wa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’ Umewasilishwa Mahakama ya Rufaa maombi ya kuitaka mahakama hiyo ipitie upya uamuzi wa Mahakama Kuu wa kukubali kusikiliza utata suala la utata huo 

Wakili wa serikali Bi. Elizabeth Kaganda alieleza hayo jana mahakamani hapo mbele ya ya Jaji Dkt. Fauz Twaib wakati shauri hilo lilipokuja kutolewa uamuzi 

Kaganda aliiambia mahakama hiyo kuwa tayari wameshawashilisha maombi hayo mahakamani hapo na kupewa namba 6/2012 hivyo aliiomba Mahakama hiyo isitoe uamuzi hadi hapo Mahakama ya rufaa itakapopitia upya maamuzi hayo 

Alidai katika maombi hayo waliyowasilisha wanaomba Mahakama ya rufaa iwape muongozo kuhusu uamuzi huo uliotolewa na Jaji huyo

Hata hivyo mmoja wa mawakili wanaomtetea Lulu alipinga maombi ya upande wa mashitaka kwa kuwa maombi hayo yamewasilishwa hatua za mwisho

Pamoja na hayo mahakama hiyo imetoa amri ya kuitaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusitisha kutaja shauli hilo hadi Mahakama Kuu itakapotoa uamuzi juu ya swala hilo

No comments:

Post a Comment