Muigizaji wa filamu wa kike na maarufu nchini Nigeria Genevieve Nnaji ameteuliwa na kampuni ya Land Rover and Coscharis Motors kuwa balozi wa Range Rover Evoque mpya nchini Nigeria.
Ushirikiano kati ya Genevieve na Land Rover ulitangazwa katika hafla iliyofanyika mwishoni mwaka wiki iliyopita mjini Lagos, Nigeria .
Muigizaji huyo anaungana na Victoria Beckham kama balozi aliyechaguliwa kuwakilisha gari aina ya Range Rover Evoque.
Range Lover aina ya Evoque ni ndogo zaidi, nyepesi na inayotumia mafuta kidogo kuwahi kutengenezwa na kampuni ya Land Lover na kwa sasa inanunuliwa rasmi nchini Nigeria.
Genevieve ambaye pia alipewa gari yake mwenyewe ya aina hiyo na rais wa Coscharis Dr. Cosmos Maduka alisema, “Ni heshima kubwa kufanya kazi na familia ya Land Rover kwenye mradi huu unaovutia. Range Rover inawakilisha ubora na umaridadi. ; Evoque inawakiklisha nguvu, class na style. Siwezi kusubiri kuiendesha!”
No comments:
Post a Comment