Mamia kwa mamia ya wapenzi na Wanachama wa timu hiyo ya Simba wakiongozwa na Mwenyekiti aliyepita MzeeHassan Dalali, Mwenyekiti wa sasa timu hiyo Mbunge wa Tabora mjini Ismail Aden Rage wameungana na viongozi wengine wa kitaifa akiwemo waziri wa habari, utamaduni na Michezo Mheshimiwa Fenelia Mkangala, Waziri Wa Afrika Mashariki Mh Samwel Sita, Mbunge wa Temeke Mh Abbas Mtemvu, Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu TFF Bwana Alfred Tibaigana, Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Lloyd Nchunga.
Aidha mandhari katika uwanja huo wa TCC Chang’ombe yalikuwa ya huzuni kubwa kwani baadhi ya wadau, wanachama na mashabiki pamoja na wachezaji mbali mbali wa timu za soka za Tanzania walibubujikwa na machozi wakati wakiutazama na kutoa heshima zao za mwisho hali iliyoongeza simanzi kwa waombolezaji.
Mchezaji Haruna Moshi Boban ndiye aliyeonekana kuumizwa zaidi na kifo cha mchezaji huyo ambaye alikuwa rafiki yake kipenzi na kushindwa kujizuia mara kwa mara pale alipoona watu wengine wakilia. Hali ilikuwa mbaya zaidi kwake pale alipoenda kutoa heshima zake za mwisho ilibidi ashikiliwe na mwenyekiti wa Klabu hiyo Mh Ismail Aden Rage.
Kwa ujumla tukio hilo la kutoa heshima na kuaga mwili wa Marehemu Mafisango lilienda vizuri ukuachilia matukio madogo madogo ya wananchi waliokuwa na taharuki ya kutaka kuwahi kuaga mwili huo wakijikuta wakipambana na askari polisi ambao walikuwepo wa kutosha na kudhibiti fujo ama matukio ya uvunjifu wa amani.
Bongo5 ilifanikiwa kuongea na ndugu wa karibu wa Marehemu Mafisango bwana Karemera Gaspas ambaye naye alikuwemo kwenye gari lilopata ajali na kusababisha kifo cha Mafisango ambaye alisema yeye alitoka na Mafisango pamoja na washikaji zao wawili na kwenda katika klabu ya usiku Maisha Club.
Tulijumuika na Bendi ya FM Academia kuanzia mida ya saa 4 usiku hadi majira ya saa 9 usiku. “ Patrick Mafisango alinipitia tukatoka pamoja na kwenda Club Maisha kuwaona FM Academia wakitumbuiza, sasa wakati tunarudi tukiwa maeneo ya Veta Changombe karibu kabisa na nyumbani kwa marehemu ilitokea Guta na Patrick alipojaribu kuikwepa gari ilimshinda na mimi nilikuja kushtuka tupo mtaroni na ndipo Mafisango alipofariki baada ya kupata majeraha mabaya usoni mwake na sehemu nyingine za mwili.
Kwa mujibu wa maelezo ya ratiba nzima ya mazishi mwili wa Patrick Mafisango unategemewa kusafirishwa kwa ndege leo jioni kuelekea jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku klabu ya Simba ikiwakilishwa na mjumbe wa kamati ya mashindano bwana Kinesi pamoja na mchezaji Haruna Moshi Boban ambaye alikuwa kipenzi chake. Mazishi yanategemewa kufanyika siku ya Jumapili huko huko Kinshasa nchini Congo.
- Baadhi ya mashabiki wa Simba wakiwa kwenye foleni kwenda kutoa heshima zao za mwisho
- Baadhi ya ndugu wa marehemu wakiwa kwenye basi
- Eric Shigongo akitoa mkono wa pole kwa Mwenyekiti wa Simba Mh. Ismail Rage
- Jamaa aliamua kujifariji kwa kuuza Jezi kama unavyo muona hapo
- Kapteni wa Simba Juma Kaseja akipewa pole na Eric Shigongo
- Karemela Gaspaz huyu alikuwa ndugu wa marehemu walikuwa wote hadi siku ya mwisho ya ajali walikuwa wote
- Mchezaji wa Simba Uhuru Selemani mwenye kizibao cheusi akiwa kwenye foleni ya kumuaga mchezajia mwezie
- Mh. Makongoro Mahanga kushoto na Mwenyekiti wa zamani wa Simba Mzee Kilomoni mwenye kofia
- Mmoja wa mashabiki akiwa mwenye huzuni sana
- Mwanachama na Mfadhili wa Simba Azim Dewiji akitoa heshima za mwisho
- Mwekiti wa Yanga Loydi Nchunga akitoa heshima zake za mwisho
- [Pichani: Mwenyekiti wa zamani wa Simba Mzee Kilomoni akiwa na Mh. Samueli Sitta] Akiongea na mwandishi wa bongo5 katika viwanja vya TCC Chang’ombe waziri wa Afrika Mashariki Mh Samwel Sita alisema msiba huu wa Mafisango uwe kichocheo kwa wachezaji waliobaki kutwaa kombe la Africa kama njia ya kumuenzi mchezaji huyo. Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Ismail Aden Rage akiongea na Bongo5 alisema kama mwenyekiti na kwa niaba ya uongozi alisema wamesikitishwa na kifo cha mchezaji huyo ambaye kwao ameacha pengo kubwa kuliziba ukizingatia mchezaji huyo alikuwa ndo mfungaji wa goli la kwanza la ligi na pia goli la Mwisho la Ligi ambalo aliwafunga Yanga.
- Mwenyekiti wa zamani wa Simba Hasani Dalali mwenye Kanzu akitoa heshima za mwisho
- Mwenyekiti wa Simba Mh.Ismail Rage akimbembeleza mmoja wa wachezaji
- Mwenyekiti wa Yanga Loydi Nnchunga akimpa pole Mwenyekiti mwenzake wa Simba Mh.Ismail Rage
- Mwenyekiti wa zamani wa Yanga Imani Madega akitoa mkono wa pole kwa mwenye kiti wa Simba Mh.Ismail Rage
- Mwili wa Marehemu Patrick Mafisango
- Shabiki huyo wa Simba alipo shindwa kujizuia hisia zake kwa huzuni aliyo nayo
- Wanamuziki wa Akudo Impact
- Waziri wa habari michezo na utamaduni Mh.Fenelia mkangala na Mwenyekiti wa Simba Mh.Ismail Adeni Rage Wakitoa Heshima za mwisho
- Wenyekiti wa zamanai wa Simba Kassim Dewiji mwenye Kanzu nyeusi na Hasani Dalali mwenye Kanzu nyeupe
No comments:
Post a Comment