Wednesday, May 30, 2012

JAY-Z, KANYE WEST KUTOKA NA KITU KIPYA




Wanamuziki vinara nchini Marekani Jay –Z na Kanye West wako mbioni kurudia tena albamu yao waliyowahi kuimba pamoja inayojulikana kwa jina la ‘Watch the Throne’ 

Kwa mujibu wa mtandao wa Spy Digital, marapa hao nguli walifyatua albamu hiyo mwaka jana ikiwa na nyimbo kama ‘Otis’ mjini Paris, Ufaransa na albamu hiyo ikafanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika orodha ya US Billboard huku ikishika nafasi ya tatu katika chati kama hiyo nchini Uingereza. 
Mtayarishaji wa albamu hiyo,Mike Dean aliliambia jarida la Quiet lunch kwamba kazi ya kuipua albamu hiyo ipo njiani.

No comments:

Post a Comment