Thursday, May 17, 2012

Kisa Cha Rais Aliyekatwa Masikio; Ni Sajenti Samuel Doe (Mwisho

Pichani ni Charles Taylor akiwa msituni.
Ndugu zangu,
Leo namalizia nilichoanza kusimulia juzi.  Charles Taylor akiwa Ivory Coast alikiandaa kikosi cha  wapiganaji  60. Kikosi kilikuwa  tayari kwa kuingia Monrovia kumwondoa Samuel Doe madarakani.
Ilikuwa ni mwaka 1989.  Wakati huo, wajuzi wa masuala ya kijeshi waliamini kabisa, kuwa Sajenti Samuel Doe angeweza , kirahisi kabisa, kumteketeza kijeshi, Charles Taylor na kikosi chake cha watu 60. Sajenti Samuel Doe angeweza kufanya hivyo hata kabla Charles Taylor hajavikaribia viunga vya Monrovia.
Badala yake, ‘ Master Sergeant’ Samuel Doe aliwatuma mstari wa mbele, wanajeshi kutoka kabila lake la Krahn.  Ni wanajeshi wa kuokoteza ambao wengine hawakuwa hata na viatu. Wanajeshi wale wa Samuel Doe, badala ya…
Pichani ni Charles Taylor akiwa msituni.
Ndugu zangu,
Leo namalizia nilichoanza kusimulia juzi.  Charles Taylor akiwa Ivory Coast alikiandaa kikosi cha  wapiganaji  60. Kikosi kilikuwa  tayari kwa kuingia Monrovia kumwondoa Samuel Doe madarakani.
Ilikuwa ni mwaka 1989.  Wakati huo, wajuzi wa masuala ya kijeshi waliamini kabisa, kuwa Sajenti Samuel Doe angeweza , kirahisi kabisa, kumteketeza kijeshi, Charles Taylor na kikosi chake cha watu 60. Sajenti Samuel Doe angeweza kufanya hivyo hata kabla Charles Taylor hajavikaribia viunga vya Monrovia.
Badala yake, ‘ Master Sergeant’ Samuel Doe aliwatuma mstari wa mbele, wanajeshi kutoka kabila lake la Krahn.  Ni wanajeshi wa kuokoteza ambao wengine hawakuwa hata na viatu. Wanajeshi wale wa Samuel Doe, badala ya kujipanga kivita, mara tu walipoiacha Monrovia na kuingia misituni, walianza kujihusisha na uporaji ikiwamo na ukataji haramu wa magogo  ya miti na kuyauza.
Taarifa ya kikosi cha Taylor kusonga mbele kutoka mpaka wa Ivory Coast na Liberia zilisambaa haraka. Vijana wengi wakaanza kujiunga na kikosi cha Charles Taylor. Jeshi la Taylor likakua kwa haraka huku likiungwa mkono na raia wengi zaidi waliokuwa na hamu ya kuuona mwisho wa utawala wa Samuel Doe.
Haikupita hata miezi sita kabla ya Taylor na vikosi vyake kukanyaga viunga vya Monrovia. Mara ikatokea,  kwenye kambi ya Taylor kukazuka mabishano baina ya makamanda. Nani aongoze shambulizi la mwisho la kuikamata Monrovia? Nani apate nini kutoka kwenye hazina ya nchi?
Mmoja wa makamanda hao alikuwa Prince Johnsson, rafiki mwingine wa zamani wa Sajenti Samuel Doe.  Urafiki wao ni  tangu Samuel Doe alipokuwa bayaye (Mlala hoi)kwenye mitaa ya Monrovia.
Katika mabishano hayo, Prince Johnsson akaamua kujitenga na Charles Taylor. Johnsson  akaunda jeshi lake. Na vita sasa ikawa ya marafiki watatu wenye  kuwania Ikulu ya Monrovia; Samuel Doe, Charles Taylor na Prince Johnsson.   
Vikawa vita vya mjini kuwania kutwaa mji na Ikulu. Mitaa ya Monrovia ikawaka moto. Raia wengi walipoteza maisha. Bayaye wa Monrovia wakawa wamejipatia kazi. Walibebeshwa silaha na kulazimika kupambana wakiwa kwenye makundi tofauti.
Ndipo vikosi vya ECOMOG  vya mataifa ya Afrika Magharibi vikiongozwa na Nigeria vikaingilia kati. Vilipiga kambi kwenye bandari ya Monrovia.
Sajenti Samuel Doe aliingizwa mjini  kwa kushawishiwa aende bandarini akakutane kwa mazungumzo ya kutafuta amani na kamanda wa vikosi vya ECOMOG.   Hiyo ilikuwa ni njama ya Prince Johnsson akishirikiana na Wa- Nigeria.
 Samuel Doe hakuwajua Wa-Nigeria. Akaamua kuchukua walinzi wake wachache na kuanza msafara wa magari aina ya Mercedes Benz kwenda bandarini kukutana na Kamanda wa vikosi vya ECOMOG.  Ilikuwa ni Septemba 9, 1990.
Samuel Doe alipofika bandarini tu, akashangaa kukutana na Prnce Johnsson na vikosi vyake. Risasi zikaanza kupigwa. Walinzi wote wa Samuel  Doe wakauawa hapo hapo.
Sajenti Samuel Doe mwenyewe akaambulia risasi za miguu na akashindwa kukimbia. Kirahisi, Samuel Doe akakamatwa. Wakamfunga kamba mikononi. Samuel Doe akaanza kuteswa.
  
Prince Johsson alimtamkia  Samuel Doe kwa kurudia rudia huku akinywa bia moja baada ya nyingine;
 "Nitajie namba ya akaunti yako”.
Kwa vile Samuel Doe hakuweza kutaja namba hiyo, Johnsson akaona kama vile hamsikii. Prince Johnsson akaamrisha; ” Mkateni masikio yake!”
Samuel Doe akakatwa masikio. Kumbe, kummkata Samuel Doe masikio hakukusaidia kumfanya asikie zaidi. Damu nyingi ikamwagika.
Tukio zima likaanza kumchosha Prince Johnnson aliyekuwa akipepewa na mwanamke kando yake.  
 Akaamuru Samuel Doe aondolewe kutoka mahali hapo. Wanajeshi wale wa Prince walimbeba Doe na kwenda naye nje. Huko waliendelea kumtesa hadi kifo chake.
Ni kipi basi kilifuatia? Na Charles Taylor ana nafasi gani katika hali hiyo mpya? Na kwa nini  marafiki hawa watatu walishindwa kubaki wamoja; Doe, Taylor na Johnsson?

No comments:

Post a Comment