Friday, May 18, 2012

Mama yake Rihanna ahamia kwa mtoto wake kwa kumhofia maisha yake

 

Maisha ya Good girl gone bad yameonekana kuchukua mkondo huo huo baada ya msanii huyo wa Kundi la Jay Z la Roc Nation kuonekana kufikia nafasi ya kua out of control kwa kula bata na kuzidisha unywaji.
Marafiki na sasa familia ya Rihanna waliokaribu naye wameonyesha wazi kutokubaliana na mwenendo wa Rihanna wa kuonekana club kila siku na kunywa pombe kupindukia, na kupelekea kulazwa hapa juzi kati kwa kutokupumzisha mwili wake inavyopasa.
Rihanna anasemekana kufuata tabia ya marehemu Whitney Houston kwa kutumia hata madawa ya kulevya na mpaka sasa wote waliokaribu naye wanamhimiza aende kupata usaidizi wa madaktari kumsaidia kuachana na masuala hayo.

Mama wa star huyo ameamua kuvalia ishu hii njuga na kuhamia nyumbani kwa Rihanna mjini Los Angeles ambapo atajaribu kumkanya na kumdhibiti mienedo ya mtoto wake huyo mwenye miaka 25.
Rihanna amedai kushangazwa na haya yote na kukanusha kwamba maisha yake yanaelekea pabaya wa kusema, yeye ni kijana mdogo na anaenjoy maisha yake bila kupretend wala kujificha.

No comments:

Post a Comment