Friday, May 18, 2012

BELLA VISTA

Mwanamume mmoja ambaye amehusishwa na shambulizi la gruneti katika mkahawa wa Bella Vista mjini Mombasa amejisalimisha kwa maafisa wa ujasusi wa CID.
Mwanamume huyo kwa jina Kassim Jembe alijisalimisha kwa maafisa hao akiwa ameandamana na wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu baada ya kutajwa na mshukiwa mkuu Jamaldin Thabit alipohojiwa na polisi.
Akiongea na wanahabari katika Afisi za mkuu wa polisi mkoani mshukiwa huyo amekanusha madai hayo na kusema kuwa alishtuka kuona jina lake kwamba anasakwa na polisi kuhusiana na ulipuaji huo uliotokea siku ya jumatatu na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine kadhaa kujeruiwa.
Jamaa huyo mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Eldoret amekiri kuwa wanajuana na mshukiwa ila kupitia kwa nduguye waliyesoma pamoja na kwamba walikutana siku ya tukio baada ya kumpigia simu na kumuarifu alikuwa hapa Mombasa.
Maafisa wa polisi kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusiana na kuhusishwa kwa jamaa huyo aliyejisalimisha.

No comments:

Post a Comment